1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

POTSDAM:Mawaziri wakutana kutayarisha mkutano mkuu wa nchi tajiri

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0w

Mawaziri wa fedha kutoka nchi nane tajiri duniani wanakutana katika mji wa Potsdam mashariki mwa Ujerumani kujadili njia za kuleta uengemavu katika masoko ya fedha.

Mawaziri hao wanakutana wakati ambapo zimebakia siku chache kabla ya mkutano mkuu wa viongozi wa nchi tajiri nane duniani utakaofanyika hapa nchini Ujerumani.Mawaziri hao pia wanazungumzia juu ya misaada kwa nchi zinazoendelea.

Wajumbe kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa pamoja na Afrika Kusini pia wanahudhuria mkutano huo wa mjini Potsdam.