1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE: Ujerumani imeifunga Jamhuri ya Czech

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFg

Ujerumani imefanikiwa kusonga mbele kugombea nafasi katika mashindano ya kandanda ya Ubingwa wa Ulaya mwaka 2008 baada ya kuikandika Jamhuri ya Czech mabao 2-1 mjini Prague.Mabao yote mawili yalitiwa na Kevin Kuranyi.Timu ya Ujerumani haikushindwa katika kundi lake,baada ya michezo mitano na sasa inaongoza kwa pointi tatu katika kundi D.