1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE: Wakazi vijijini hawataki makombora ya Marekani

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvC

Mpango wa Marekani wa kutaka kuweka sehemu ya makombora yake ya ulinzi katika Jamhuri ya Czech, barani Ulaya,umekataliwa na wakazi wa vijiji vitatu vilivyo karibu na eneo lililopendekezwa kutumiwa kuweka rada za Marekani.Mpango huo umepingwa kwa zaidi ya asilimia 90 katika kura ya maoni.Matokeo hayo ambayo hayana uzito wa kudai yatekelezwe,yametoka siku mbili kabla ya Rais George W.Bush kutembelea mji mkuu Prague.Kwa upande mwingine,Rais Vladimir Putin wa Urusi, mara nyingine tena,amesisitiza upinzani wake kuhusu mpango huo wa Marekani wa kutaka kuweka makombora ya kinga barani Ulaya.Katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani,”Der Spiegel” Rais Putin alisema,makombora hayo yanalengwa dhidi ya “kitu kisichokuwepo”.Marekani lakini inadai kuwa mataifa kama vile Iran ambayo humiliki makombora, ni kitisho.Juma lijalo wote Bush na Putin, watahudhuria mkutano wa kilele wa kundi la nchi nane tajiri zilizoendelea kiviwanda G-8 mjini Heiligendamm,kaskazini mwa Ujerumani.