1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA. Afrika Kusini yafaa kupata kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6p

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh amesema kwamba Afrika Kusini inastahili kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa

Aliwaambia waandishi wa habari mjini Pretoria kwamba kutokana na hadhi yake na mchango inayotoa katika Afrika na katika jamii ya kimataifa Afrika Kusini ina haki ya jambo hilo.

Rais Mbeki hivi karibuni alitangaza kwamba Afrika Kusini itachukua kiti cha uanachama usiokuwa wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kutoka januari mosi mwakani.

Manmohan Singh na Thabo Mbeki leo walifanya mazungumzo ya pamoja na mada walizozigusia ni marekebisho ya umoja wa mataifa pamoja na baraza lake la usalama ambapo nchi kama India, Afrika Kusini,Brazil,Japan na Ujerumani zimeelezea kutaka kuwa wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.