1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA:Kansela wa Ujerumani amekutana na rais Mbeki

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IJ

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewasili nchini Afrika Kusini kituo cha pili cha ziara yake barani Afrika.

Akiwa mjini Pretoria amefanya mazungunzo na mwenyeji wake rais Thabo Mbeki.

Kansela Angela Merkel katika mazungumzo yao amemtaka rais Mbeki amtie kishindo rais Mugabe wa Zimbabwe.

Kiongozi huyo amepokea pia maelezo kuhusu maandalizi ya kombe la dunia la kabumbu yatakayofanyika mwaka 2012 nchini Afrika Kusini.

Kabla ya hapo kansela Merkel alikuwa nchini Ethiopia ambako aliitolea mwito jumuiya ya kimataifa itathmini upya uhusiano wake na bara la Afrika.

Akiwahutubia wawakilishi wa umoja wa Afrika mjini Addis Ababa kansela Angela Merkel amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa uhusiano kati ya Umoja wa ulaya na na bara la Afrika na wakati huo huo amehimiza juu ya kuheshimiwa haki za binadamu.