1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA:Ujerumani kuisaidia Afrika Kusini kuandaa kombe la dunia

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IC

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani yuko nchini Afrika Kusini kituo cha pili cha ziara yake barani Afrika.

Akiwa mjini Pretoria amefanya mazungunzo na mwenyeji wake rais Thabo Mbeki. Mazungumzo yao yamegusia hali ya nchini Zimabbwe na jinsi jumuiya ya kimataifa inavyo weza kuishinikiza nchi hiyo jirani ya Afrika Kusini iheshimu haki za binadamu.

Kuhusiana na hali ya nchini Zimabbwe kansela Angela Merkel amesema.

Afrika Kusini ni mpatanishi kati ya serikali ya rais Robert Mugabe na upande wa upinzani.

Kansela Angela Merkal anatarajiwa pia kuzuru uwanja unaojengwa mjini Johannesburg kwa ajili ya fainali ya kombe la dunia la kabumbu itakayofanyika mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

Bibi Merkel amemuhakikishia rais Thabo Mbeki kwamba Ujerumani itaiunga mkono Afrika Kusini katika maandalizi ya michuano hiyo.

Kansela Angela Merkel amesisitiza umuhimu wa kuimarishwa uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na bara la Afrika na wakati huo huo amehimiza juu ya kuheshimiwa haki za binadamu.