1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pristina. Kosovo huenda ikagawanywa.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZb

Kundi la mataifa makubwa linalofanya mazungumzo juu ya jimbo la Kosovo limesema kuwa hawaondoi tena uwezekano wa kuligawa jimbo hilo la Serbia.

Akizungumza katika mji wa Pristina , mwanadiplomasia wa Ujerumani Wolfgang Ischinger , ambaye ni mwakilishi wa umoja wa Ulaya, amesema kuwa kila uwezekano ulijadiliwa baada ya majadiliano ya mwishoni mwa juma kushindwa kuleta makubaliano baina ya viongozi wa Kosovo na Serbia.

Kundi hilo la mataifa , ambapo linajumuisha wawakilishi kutoka Russia na Marekani limepewa hadi Desemba mwaka huu kujaribu kufikia makubaliano kamili ya hali ya baadaye ya Kosovo.

Serbia imekataa pendekezo la umoja wa mataifa ambalo lingeipatia uhuru Kosovo.

Russia imetishia kutumia kura yake ya turufu katika kuzuwia juhudi zozote za utkelezaji wa mpango huo.