1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRISTINA: Waalbania 1,000 waandamana

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDV

Waalbania takriban 1,000 katika jimbo la Kosovo wamefanya maandamano ya kupinga mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya baadaye ya jimbo hilo.

Maandamano hayo yaliandaliwa na kundi la vijana wa Albania, liitwalo Self Determination, linalotaka jimbo la Kosovo liwe huru kutoka kwa Serbia bila mashauriano yatakayoijumulisha serikali ya Serbia mjini Belgrade.

Kundi hilo linasema linaupinga mpango uliopendekezwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Mahtti Ahtisaari, ingawa mpango huo unalipa jimbo la Kosovo uhuru utakaosimamiwa.

Mkoa wa Kosovo umekuwa ukitawaliwa na tume ya Umoja wa Mataifa tangu katikati ya mwaka wa 1999 baada ya kampeni ya mabomu iliyofanywa na jeshi la shirika la kujihami la kambi ya magharibi, NATO, kumaliza mauaji ya Walbania walio wengi yaliyofanywa na wanajeshi wa Serbia.

Baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zinaupinga mpango huo wa Umoja wa Mataifa zikiwemo Slovakia, Ugiriki, Uhispania, Slovenia na Romania.