1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prodi afanya ziara Afghanistan.

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfdn

Kabul.

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi amefanya ziara nchini Afghanistan , akiwa kiongozi wa tatu kutoka mataifa ya magharibi kufanya ziara hiyo wiki hii. Prodi amekutana na rais Hamid Karzai wa Afghanistan na jenerali Dan McNeill, kamanda wa majeshi yanayoongozwa na NATO yanayopambana na wapiganaji wa Taliban nchini humo. Pia alikwenda katika mji wa magharibi wa Herat ambako wengi wa wanajeshi wa Italia wapatao 2,300 wako. Prodi amesema kuwa Afghanistan inahitaji msaada kutoka jumuiya ya kimataifa. Ziara yake inafuatia ziara ya rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu mpya wa Australia Kevin Rudd.