1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRSTINA : Waandamana kupinga mpango wa Umoja wa Mataifa

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMe

Maelfu ya watu wa asili ya Albania wameandamana katika mjii mkuu wa Kosovo Pristina kupinga mpango wa Umoja wa Mataifa juu ya mustakbali wa jimbo hilo la Serbia.

Waandamanaji walikuwa wakitowa kauli mbiu dhidi ya Umoja wa Mataifa na kupeperusha bendera za Albania pamoja na kubeba maberamu ya kudai haki ya kujitawala.

Kosovo imekuwa chini ya utawala wa Umoja wa Mataifa tokea mashambulizi ya mabomu ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO kukomesha mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Yugoslavia na watu wa asili ya Albania hapo mwaka 1999.Mpango huo wa Umoja wa Mataifa utaipa Kosovo nishani zote za kuwa taifa lakini sio uhuru rasmi.

Wananchi wa asili ya Albania ambao ndio walio wengi katika jimbo hilo wanasema pendekezo hilo halitoshelezi wakati maafisa wa serikali ya Serbia wanasema katu hawatokubali Kosovo kupewa uhuru.