1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PSG, Benfica zapata ushindi Champions League

17 Februari 2016

Michuano ya hatua ya 16 ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya ilirejea jana usiku, ambapo nchini Ufaransa Paris Saint Germain iliiwafunga wageni Chelsea mabao mawili kwa moja

https://p.dw.com/p/1HwWr
UEFA Champions League Paris Saint Germain - FC Chelsea
Picha: picture-alliance/dpa/Y. Valat

Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani ndio walioifungia PSG mabao wakati John Obi Mikel akiifungia Chelsea na kuipa matumaini ya kupeleka nyumbani London faida ya goli la ugenini ambalo huenda likawasaidia katika mchuano wa marudiano mnamo Machi 9. Kocha wa Chelsea Guus Hiddink amesema watajaribu kuitumia vyema faida ya goli la ugenini isipokuwa amekiri kuwa PSG ina kikosi thabiti ambacho kina uwezo mkubwa wa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali

Katika mchuano mwingine Benfica ilihitaji bao la dakika ya mwisho lililofungwa kwa njia ya kichwa na Jonas ili kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya zenit St Petersburg mjini Lisbon. Bao hilo lilifungwa katika muda wa majeruhi baada ya mchezaji wa Zenit Domenico Criscito kupewa kadi ya pili ya njano na hivyo kutimuliwa uwanjani.

Leo usiku, klabu ya Ujerumani Wolfsburg itakuwa ugenini kupambana na Gent ya Ubelgiji wakati Miamba wa Uhispania Real Madrid wakicheza ugenini Italia dhidi ya AS Roma.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Daniel Gakuba