1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Purukushani zaendelea Uganda

15 Aprili 2011

Zaidi ya watu 220 wamekamatwa katika baadhi ya maeneo nchini Uganda na wengine kadhaa wamejeruhiwa kutokana na maandamano yanayoendelea.

https://p.dw.com/p/10tx8
Ramani ya UgandaPicha: DW

Hata hivyo baadhi ya sehemu zinaripotiwa kuwa tulivu, tarifa ambazo zimethibitishwa pia na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Hapo jana polisi nchini humo walimzuwia kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye kwa tuhuma za kuyaongoza maandamano mjini Kampala ikiwa ni siku tatu tangu ajaribu kufanya hivyo. Itakumbukwa kuwa kiongozi huyo alikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwasababu ya tuhuma za kufanya maandamano kinyume na sheria. Polisi walifyatua risasi na kuwarushia makopo ya gesi ya machozi waandamanaji waliokuwa wamekusanyika nchini humo. Dhamira ya maandamano hayo ni kupinga ongezeko la bei za bidhaa muhimu za matumizi.

Mhariri: Charo,Josephat