1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin afanya ziara ya kushtukiza Mariupol na Crimea

19 Machi 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin jana amefanya ziara ya kushtukiza katika rasi ya Crimea katika kuadhimisha miaka tisa tangu alipoinyakua kutoka Ukraine.

https://p.dw.com/p/4OtqH
EU-Sanktionen gegen Russland
Picha: Mikhail Metzel/Sputnik/AFP/Getty Images

Putin aliutembelea pia mji wa Ukraine wa Mariupol unaokaliwa kimabavu. Ziara ya Putin inajiri siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kutoa waranti wa kukamatwa kwake kwa uhalifu wa kivita, ikimtuhumu kwa uwajibikaji katika utekaji nyara wa watoto nchini Ukraine.

Soma pia:ICC yataka Putin akamatwe 

Moscow imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama hiyo. Kyiv inasema tangu kuanza kwa uvamizi huo Februari 2022, zaidi ya watoto 16,000 wa Ukraine walihamishwa kinyume cha sheria kuelekea Urusi. Wakati huo huo, mapigano makali yanaendelea huko Donetsk hasa katika mji wa Bakhmut.