1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais Vladimir Putin kushiriki mkutano wa kilele wa G 20

Lilian Mtono
19 Novemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin atashiriki katika mkutano wa kilele wa viongozi wa Kundi la Mataifa yaliyoinukia na yanayoinukia kiuchumi - G20 kwa njia ya mtandao siku ya Juamatano.

https://p.dw.com/p/4Z9Ah
Kasachstan | Vladimir Putin azuru Astana
Rais Vladimir Putin anatarajiwa kushiriki kwenye Mkutano wa Kilele wa kundi la G20 utakaofanyika kwa mtandaoPicha: Konstantin Zavrazhin/AFP/Getty Images

Putin anashiriki mkutano huu, baada ya kushindwa kushiriki mkutano wa ana kwa ana huko New Delhi mnamo mwezi Septemba.

Kituo cha Televisheni cha Urusi cha Vesti kimearifu hayo katika chapisho lake la matandao wa kijamii mapema leo.

Putin hakuhudhuria mkutano miwili ya G20 iliaoyoandaliwa na India mwezi Septemba na Indonesia mwaka uliopita, ambako alimtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov.

Kiongozi huyo amesafiri mara chache nje ya nchi yake tangu Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu, ICC ilipotoa waranti wa kumkamata kwa makosa ya kuwahamisha kinyume cha sheria watoto wa Ukraine.