1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONG-YANG:Korea Kaskazini yashutumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6H

Nchi zenye nguvu duniani zimepinga vikali kitisho cha Korea Kaskazini cha kutaka kufanya majaribio ya makombora yake ya kinuklia.

Marekani imesema kuwa majaribio hayo yatakuwa ni kitendo cha uchochezi na huenda yakasababisha madhara kwa utawala wa kikomunisti.

Umoja wa Ulaya,Urussi Japan na China wameitaka serikali ya mjini Pyongyang kujizuia kufanya hivyo na kutohujumu usalama wa eneo hilo na kimataifa kwa jumla.

Kwa upande wake Korea Kusini imesema haitoruhusu majaribio hayo ya mabomu ya Korea kaskazini kufanyika na imeitaka nchi hiyo kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesema Korea Kaskazini itakabiliwa na lawama za ulimwengu mzima endapo itafanya majaribio hayo ya silaha za kinuklia.

Hata hivyo Korea Kaskazini haijasema lini majaribio hayo yatafanyika lakini imesema itafanya hivyo kukabiliana na ongezeko la uhasama wa Marekani.