1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONG YOUNG: Korea ya kaskazini yasema itafanya jaribio la kinyuklia

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6T

Korea ya kaskazini imetangaza kuwa itafanya jaribio la kombora la kinyuklia kuimarisha ulinzi wake kufuatia kile imekitaja kuzidi vitisho vya Marekani dhidi yake. Tamko hilo limetolewa na waziri wa mambo ya kigeni na kutangazwa na shirika la habari la taifa. Japan tayari imetoa maneno makali kwamba huo ni mpango usiyovumiliwa ikitishia hata kuchukuwa hatua kali. Korea ya kaskazini inasema kuwa ilitengeneza silaha za kinyuklia ila kwamba hadi sasa ilikuwa haijafanya jaribio lolote kuthibitisha kuwa inazo silaha za aina hiyo.