1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: Muda wa kufunga kinu cha nyuklia wamalizika

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9w

Muda wa mwisho hadi Korea Kaskazini iwe imefunga kinu chake cha nyuklia cha Yongbyon umemalizika huku nchi hiyo ikiwa bado haijatimiza azimio hilo.

Makubaliano ya pande sita yaliafikiwa mwezi Februari lakini Korea Kaskazini ilifahamisha kwamba haitafunga kinu chake hicho hadi pale Marekani itakapotimiza ahadi ya kuachiliwa fedha zilizozuiliwa katika benki ya Macau ya China.

Marekani imesema kwamba Korea kaskazini inajiburuza katika zoezi hilo la kukifunga kinu cha nyuklia cha Yongbyon.

Mjumbe wa Marekani katika mazungumzo hayo ya nyuklia Christopher Hill amesema kwamba atakutana na mwenziwe wa China leo ili kutafakari mustakabali wa mzozo huo.