1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qatar yashindwa kuyapanisha makundi hasimu ya Wapalestina

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4D

Qatar imesema kuwa hadi sasa haijafanikiwa kuyapatanisha makundi hasimu ya kipalestina. Waziri wa mambo ya kigeni wa Qatar, Sheikh Hamad bin Jassen bin Jabr al- Thani, alisema akitokea katika mazungumzo kwenye ukanda wa Gaza kwamba hadi sasa tofauti zimesalia.

Chama tawala chenye msimamo mkali huko Palestina cha Hamas hadi sasa kimepinga kuitambua Israeli. Hilo lilikuwa moja kati ya masharti ya nchi za magharibi ambazo zilisimamisha misaada kwa serikali yenye kuongozwa na Hamas mara tu baada ya kuchaguliwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.