1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

QUETTA: Shambulio la bomu ndani ya mahakama

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRL

Si chini ya watu 15 wameuawa na wengi wengine wamejeruhiwa,baada ya bomu kuripuka mahakamani katika mji wa Quetta kusini-magharibi mwa Pakistan.Kwa mujibu wa polisi,bomu hilo liliripuka wakati ambapo kesi moja ilikuwa ikiendelea.Ripoti zisizothibitishwa zinasema,jaji na idadi fulani ya mawakili ni miongoni mwa wale waliofariki.Polisi inatuhumu hilo ni shambulio la kujitolea muhanga.Mji wa Quetta,unajulikana kama ni kituo muhimu cha harakati za wanamgambo wa Kitaliban wa nchi jirani Afghanistan.Vile vile katika wilaya ya Baluchistan kumetokea mashambulio mengi ya kigaidi,tangu kiongozi wa waasi wa eneo hilo kukamatwa mwezi wa Agosti mwaka 2006.