1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT: Chama cha PJD kinatazamia kushinda

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSr

Chama Kikuu cha Kiislamu cha PJD nchini Moroko, kinatumaini kupata ushindi mkubwa katika chaguzi za bunge zitakazofanywa siku ya Ijumaa.Uchunguzi wa maoni uliofanywa mwezi uliopita,unaashiria kuwa PJD kipo mbele ya vyama hasimu viwili: Istiqlal na USFP.Hivi sasa,chama cha kizalendo cha Istiqlal,kina viti 50 bungeni na ni mshirika mkuu katika serikali ya mseto nchini Moroko.Chama cha Wasoshalisti USFP,ni chama kikuu cha pili kikiwa na viti 48 na kinafuatwa na chama cha Kiislamu cha PJD chenye wabunge 42.Uchaguzi wa bunge utakaofanywa tarehe 7 Septemba unagombewa na vyama 33.