1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT: Watu wawili wajitoa muhanga

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9v

Watu wawili wamejitoa muhanga kwa kujilipua kwa mabomu katikati ya barabara kwenye eneo kilipo kituo cha utamaduni cha Marekani mjini Casablanca nchini Moroko.

Afisa wa wizara ya mambo ya ndani amesema kuwa katika shambulio hilo watu hao waliuwawa papo hapo na mwanamke mmoja amejeruhiwa.

Maeneo yaliyotokea shambulio hilo ni karibu pia na benki katika barabara ya Moulay Youssef mjini Casablanca.

Polisi imetoa taarifa kwamba watu hao waliojitoa muhanga hawakuwa wakifuatwa na polisi.