1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia mmoja wa Ujerumani akamatwa kuhusiana na mpango wa nuklia wa Iran

17 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cr6s

BERLIN:

Raia mmoja wa Ujerumani, mwenye asili ya Iran, amekamatwa mjini Berlin kwa kushukiwa kujaribu kusafirisha nje kwa siri,vifaa muhimu kwa mpango wa tatanishi wa Nuklia wa Iran.

Wendesha mashtaka wa Ujerumani wamesema kuwa mtu huyo, mwenye umri wa miaka 52, anashtumiwa kwa kwenda kinyume na marufuku iliowekwa,alipojaribu kutoa, kile kilichoitwa -vyombo muafaka kwa Nuklia -kwa mtambo ambao unajihusisha na shughuli za atomik za Iran.Duru za karibu na uchunguzi zinasema kuwa, vifaa vinavyozumzwa hapa ni kemikali na wala sio Nuklia.Mataifa matano ambayo ndio wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, mkiwemo Ujerumani,yanajaribu kukubaliana kuhusu kutekeleza vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, kwa kukaidi miito ya kusitisha kazi za urukurutubishaji madini ya Uranium katika mitambo yake ya nuklia.