1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Zambia Wapiga Kura.

Ponda, Eric Kalume29 Oktoba 2008

Wazambia wanapiga kura Alhamisi kumchagua rais mpya baada ya kifo cha Rais Levy Mwanawasa Agosti mwaka huu. Wagombea ni makamu wa Rais Ruphia Banda wa wa chama cha PF na Micheal Sata wa MMD

https://p.dw.com/p/Fjne
Wananchi wa Zambia katika mkutano mmoja wa Kampeni za uchaguzi wa Urais unaofanyika Alhamisi.Picha: DW


Serikali imeweka ulinzi mkali baada ya Bw Sata kutamka kwamba hatoyakubali matokeo iwapo akishindwa, akiashiri juu ya vitendo vya udanganyifu wa kura.


Viongozi hao wawili waliimarisha kamepini zao katika maeneo mbali mbali ya mji mkuu Lusaka, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Alhamisi, ambao umetajwa kuwa kinyang´anyiro baina ya vigogo hao viwili wa kisiasa, ingawa bado kunawagombea wengine wawili wanaoshiriki uchaguzi huo.


Hata hivyo Micheal Sata ambaye ameshiriki na kushindwa katika chaguzi mbili zilizopita, mwaka wa 2001 na pia 2006, amekanusha madai kwamba anapanga kuchochea ghasia iwapo atashindwa kwenye uchaguzi wa leo.


Kulingana na kura ya maoni iliyotolewa jana na shirika la kibinafsi, Micheal Sata anaongoza kwa karibu dhidi ya Banda, ingawa kwa upande mwengine, matokeo ya kura ya maoni yaliyotolewa na gazeti la serikali, yalionyesha kuwa Banda alikuwa akiongozwa kwa kati ya asilimia 42 na 46 dhidi ya Sata alie na kati ya asilimia 31 na 35.


Hii si mara ya kwanza kwa Sata kutoa vitisho vya kutoyakubali matokeo ya uchaguzi, kwani mara ya kwanza mwaka wa 2006, matanshi hayo yalizua ghasia katika barabara za Mji wa Lusaka.


Wakati wa ghasia hizo, wafusi wa Sata walifunga barabara, kurushia magari mawe na kuvunja maduka mjini humo, kupinga kuchaguliwa kwa Rais Mwanawasa.


Tangazo la Michale Sata la kutoyakubali matokeo ya uchaguzi, linafuatia kisa cha mwezi uliopita, ambapo kunamadai kwamba Gari la serikali lilinafumaniwa likisafirisha makaratasi ya kupigia kura hadi wilaya moja katika jimbo la Kusini nchini humo.


Yasemekana wafuasi wa Bw Sata walifunga barabara na kuliharibu gari hilo lililokuwa makaratasi ya kura yaliyowekwa alama ya Rupia Banda, ingawa maafisa wa serikali wamekanusha dai hilo wakisema kuwa gari hilo lilikuwa likisafirisha taa na Betri vitakavyotumiwa wakati wa uchaguzi.


Banda mwenye umri wa miaka 71, ambaye katika kampeini zake anahidi kuendeleza sera na maongozi ya mtangulizi wake Levy Mwanwasa, anasema kuwa ataimarisha uchumi wa taifa hilo ambalo zaidi ya asilimia 60 ya wakaazi wake wanaishi chini ya Dola mbili kwa siku.


Wakati wa utawala wa Mwanwasa, uchumi wa nchi hiyo ulikuwa kwa kiwango cha kadri kutokana na kushuka kwa biashara ya Almasi ambayo ni tegemeo kubwa la uchumi wa taifa hilo.

Bei ya Almasi imeshuka kwa kiwango cha asilimia 50 tangu mwezi Julai hali inayozua hofu kuhusu hali ya uchumi wa taifa hilo katika siku za usoni.


Kwa upande wake Micheal Sata anaahidi kufanya mabadiliko katika muda wa siku 90 za kwanza madarakani, miongoni mwayo ikiwa ni kulazimisha kampuni za kigeni kutoa asilimia 25 ya hisa zao kwa waekezaji raia wa nchi hiyo.


Mbali na hayo anaahidi kuboresha makaazi na kubuni nafasi zaidi za ajira kwa raia wake.


Wagombea wengine wawili ni Hakainde Hichilema wa chama cha UPND na Godfrey Miyanda wa chama cha Heritage.