1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Abbas hataki mazungumzo na Hamas

21 Juni 2007

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa hatafanya mazungumzo na chama cha Hamas na amemlaumu kiongozi wa chama hicho Khaled Mashaal anaeishi nje ya Palestina kwa kula njama za kutaka kumwuua.

https://p.dw.com/p/CB3S
Rais wa Mamlaka ya Palestina, M.Abbas
Rais wa Mamlaka ya Palestina, M.AbbasPicha: AP

Akizungumza kwenye makao makuu ya serikali katika mji wa Ramallah,kwenye ukingo wa magharibi, bwana Abbas amesema kuwa chama cha Hamas ni kundi la wauaji na magaidi waliopanga kumwuua.

Pia amewashutumu watu wa nje kwa kushirikiana na Hamas katika kutekeleza mpango wa kukitimua chama chake kutoka Gaza.

Rais Abbas pia ameitaka jumuiya ya kimataifa ifufue mazungumzo ya kuleta amani katika mashariki ya kati.