1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ahmadinejad aunga mko kuwepo kwa mataifa ya Israel na Palestina

Jason Nyakundi27 Aprili 2009

Iran iko tayari kwa mazungumzo ya nuklia

https://p.dw.com/p/Hf3j
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad.Picha: AP

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema litakuwa jambo zuri kwao ikiwa kutafikiwa makubaliano ya amani ya kuwepo mataifa mawili Israel na Palestina. Matamshi hayo ya rais wa Iran yamekuja baada ya Hii inakuja baada ya wajumbe kutoka nchi za Ulaya kuondoka kwenye mkutano wa kupinga ubaguzi ulioandaliwa mjini Geneva, nchini Uswisi hivi karibuni, kutokana na matamshi ya rais Ahmedinejad dhidi ya Israel.

Kupitia mahojiano yaliyopeperushwa na kituo cha runinga cha Marekani ABC , rais Ahmadinejad alionekana kutofurahishwa na uamuzi wa rais wa Marekani, Barack Obama, wa kukataa kujibu ujumbe wake wa salamu na kuongeza kuwa mazungumzo ya nuklia yataendelea tu ikiwa kutakuwa na ajenda kuu.

Akitoa hotuba kwenye mkutano wa kupinga ubaguzi uliondaliwa mjini Geneva, nchini Uswisi, rais Ahmadinejad alikishutumu kile ambacho alikitaja kuwa hatua ya rais Obama ya kuunga mkono mauaji ya raia wa Ukanda wa Gaza.

Hata baada ya kutoa wito wa kuitaka Israel iondolewa kwenye ramani ya dunia, wakati huu rais Ahmadinejad alionekana kubadili msimamo na kutaka kuwepo kwa taifa la Palestina kando na taifa la Israel na adui wake mkubwa.

"Uamuzi wowote watakaochukua litakuwa jambo zuri kwetu na tutauunga mkono", alisema rais Ahmadinejad.

Katika mkutano wa kupinga ubaguzi mjini Geneva, rais Ahmadinejad alitoa hotuba iliyosababisha ujumbe kutoka nchi za Ulaya kuondoka mkutanoni, huku Marekani na Israel zikiususia mkutano huo.

Akiushutumu uamuzi wa Marekani wa kutoshiriki kwenye mkutano huo, rais Ahmadinejad alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa Geneva lilikuwa ni kutafuta njia za kuumaliza ubaguzi.

Kernkraftwerk Iran
Kinu cha nuklia cha Bushehr nchini Iran.Picha: picture alliance / abaca

Kwenye mahojiano hayo ya siku ya Jumapili, hata hivyo, Rais Ahmadinejad alisema kuwa ni jukumu la Marekani kuwa kwenye mstari wa mbele kwenye mazungumzo kuhusu mpango wa nyukilia ambao mataifa ya magharibi yanadai kuwa una lengo la kuunda silaha za nuklia.

Ahmadinejad alisema kuwa amepata kushutumiwa nchini mwake baada ya kumtumia pongezi rais Obama alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani, lakini akaongeza kuwa bado anasubiri majibu.

Mwezi ukliopita rais Obama alilitumia taifa la Iran ujumbe wa mwaka mpya ambapo alitoa wito wa kuwepo mwanzo mpyakatika uhusiano kati ya Marekani na taifa hilo la kiisklamu baada ya miongo mitatu ya uhusiano mbaya kati yao.

Wiki iliyopita waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Hilarry Clinton, alisema kuwa Marekani ilikuwa ikiandaa vikwazo vikali dhidi ya Iran ikiwa juhudi mpya za Marekani za kutafuta maelewano zitashindwa kuzaa matunda.

Mapema mwezi uliopita rais Ahmadinejad alisema kuwa Iran itatoa habari kuhusu mpango wake wa nyuklia kwa mataifa yenye nguvu duniani na kuongoza kuwa Iran iko tayari kwa mazungumzo.

Naye mfalme wa Jordan, Abdullah wa Pili, kwenye mahojiano na kutuo cha runinga cha Marekani, jana jumapili alisema kuwa utawala wa rais Obama ni lazima utafute njia za kutatua suala la nyukilia la Iran pamoja na lile la kupatikana amani matika eneo la Mashariki ya Kati.

Mwandishi: Jason Nyakundi/AFP

Mhariri:M.Abdul-Rahman.