1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais al-Sisi wa Misri ziarani Tanzania

15 Agosti 2017

Abdel Fattah al-Sisi amekamilisha ziara yake ya siku mbili Tanzania, huku ajenda ya kuutafutia ufumbuzi mzozo wa matumizi ya Mto Nile ikiwa moja ya mambo aliyokubaliana nayo na mwenyeji wake, Rais Magufuli.

https://p.dw.com/p/2iDyV
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi na mwenyeji wake John Magufuli
Picha: Reuters/E.Herman

J2 15.08.2017 Tansania- Fatah al Sissi und Magufuli über Nil-Konflikt - MP3-Stereo

Baada ya kutoka Tanzania, al-Sisi ameelekea Rwanda kwa ziara ya siku mbili nchini humo. Balozi wa Misiri nchini Rwanda Namira Negm amesema zira hii inalenga kuleta ukurasa mpya baina ya Misri na nchi nyingine za kiafrika. Rais Sisi amekwenda Rwanda baada ya Tanzania katika ziara ambayo itampeleka pia kwenye nchi za Chad na Gabon.