1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Assad aapishwa kuchukua hatamu kipindi cha pili nchini Syria

Mohammed Abdul-Rahman17 Julai 2007

Ameitaka Israel itowe jibu kuhusiana na pendekezo la amani kutoka Syria, akisema nchi yake haitaki mazungumzo ya siri, badala yake viongozi wa Israel watamke bayana nia yao kuhusu amani.

https://p.dw.com/p/CHAu
Rais Beshar al-assad wa Syria.
Rais Beshar al-assad wa Syria.Picha: AP

Rais Beshar al-Assad alisema Syria inataka viongozi wa Israel watowe hakikisho kwamba ardhi yake yote inayokaliwa, akiongeza hawawezi kuingia katika mazungumzo bila kujua kitakachojadiliwa .

Kiongozi huyo wa Syria alikua akilihutubia bunge mjini Damascus, baada ya kuapishwa kwa kipindi cha pili cha uongozi. Assad mwenye umri wa miaka 41 alichaguliwa tena mwezi Mei katika kura ya maoni ambapo alikaua mgombea pekee na kutangazwa kuwa amejinyakulia ushindi wa asili mia 97 ya waliopiga kura. Kadhalika ameahidi kuendelea na mageuzi ya kiuchumi, ikiwa ni katika wakati ambao Syria inakabiliwa na mbinyo wa Marekani kuhusiana na kuhusika kwake katika migogoro ya Lebanon na Irak.

Marekani iliiwekea Syria vikwazo vya kiuchumi kwa sababu ya sera zake kuelekea Lebanon na Irak. Na Assad amekumbwa pia na shindikizo kubwa la kimataifa tangu Februari 2005 baada ya kuuwawa Waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq hariri mjini Beirut, mji ambao wakati huo ulikua chini ya usimamizi wa wasyria, iliokua na majeshi nchini Lebanon.

Mazungumzo ya moja kwa moja na Israel yamesita tangu Januari 2000, huku Syria ikidai kurejeshewa miliama ya Golan inayokaliwa na Israel baada ya kuiteka wakati wa vita vya siku sita 1967 na kulitwaa eneo hilo 1981.

Sehemu ya kwanza ya hotuba ya Assad leo ilituwama zaidi katika maswala ya ndani akiahidi pia kuwalinda masikini na wasio na nafasi kimaisha. Ushindi uliotangazawa baada ya kura hiyo ya maoni ulishatabiriwa na vyama vya upinzani vilivyoisusia vikisema matokeo yameshapangwa na yanajulikana tangu mapema.

Wakati kiongozi huyo wa Syria akimtaka hasimu yake Israel itamke wazi nia yake kuhusu amani, dola hiyo ya kiyahudi kwa upande mwengine imechuzkua hatua nyengine leo katika safu ya kusaka amani na wapalestina.

Kamati ya mawaziri ya Israel leo iliidhinisha orodha ya zaidi ya wafungwa 200 wa kipalestina watakaoachiwa huru, ikiwa ni ishara njema kwa rais Mahmoud Abbas. Taarifa zilisema wafungwa 256 wanatarajiwa kuachiwa huru Ijumaa ijayo. Katika orodha hiyo yumo pia Abderahim Malluh, naibu mkuu wa chama cha ukombozi wa umma wa palestina – Popular Front for the Liberation of Palestine-PFLP.

Malluh mwenye umri wa miaka 60 na mmoja wa waanzilishi wa chama hicho ,alikamatwa 2002 na kuhukumiwa kifungo cha miaka 9 jela na mahakama ya kijeshi ya Israel miaka miwili baadae, kwa kuhusika na kile kilichoelezwa kuwa ni kundi la kigaidi.

Pia kiongozi wa PFLP Ahmed Saadat alikamatwa 2001 , baada ya kundi hilo kumuuwa aliyekua waziri wa utalii wa Israel Rehavem Zeevi. Kuna wafungwa zaidi ya 11,000 wakipalestina katika jela za Israel