1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush ahutubia mkutano mkuu wa chama cha Republican

3 Septemba 2008

-

https://p.dw.com/p/FANI
Asema McCain anajali na kuyathamini maisha ya wanadamuPicha: AP

Rais George W Bush ametoa hotuba yake katika mkutano mkuu wa chama cha Republican kupitia njia ya Satellite na kumuidhinisha rasmi John McCain kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican akisema kwamba ni mtu aliye tayari kuliongoza taifa la Marekani na kufanya maamuzi magumu yanayohitajika katika ulimwengu huu hatari.Bush amesema.

''Tunaishi katika ulimwengu hatari na tunahitaji rais anayeelewa mafunzo yaliyotokana na mashambulio ya Sept 11 mwaka 2001 kwamba inabidi kuilinda Marekani,tuitetee,kuzuia mashambulio kabla hayajatokea na kutosubiri kushambuliwa tena.Kwa hivyo mtu tunayemuhitaji ni John McCain''

Bush pia amemsifu John McCain kuwa ni mtu anayejali na kuthamini maisha ya wanadamu na ndio sababu yuko tayari kuitetea nchi.

Amemtaja McCain kuwa mtu jasiri aliyejitolea kuyahatarisha matumaini yake ya kisiasa ya kuingia ikulu ya White House kwa kuunga mkono vita vya Iraq.

Amewataka wananchi wa Marekani kumpigia kura McCain ili kuiendeleza mbele Marekani.

John McCaina anatazamiwa kukubali rasmi uteuzi wa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican hapo kesho.

Kwa upande mwingine warepublican wamemtetea mgombea mwenza wa McCain Sarah Palin wakati akiandamwa na kashfa mpya ya rushwa.