1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush akabiliwa na kishindo bungeni

Omar Mutasa11 Mei 2007

Baraza la wawakilishi katika bunge la Marekani -Congress lakataa kuidhinisha fedha ailizoshauri rais Bush

https://p.dw.com/p/CB4A
Spika wa bunge la Marekani-.Congress
Spika wa bunge la Marekani-.CongressPicha: AP

Baraza la waakilishi katika baraza la Kongress la US wamemtaka Rais George Bush kabla ya mwezi wa july aweze kuwathibitisha kua hali ya Askari wa Mmerekani nchini Iraq itakua ya usalama zaidi, ndipo waakilishi hao watakapo weza kuidhinisha Fedha alizoomba Bush kwa ajili ya Askari wa kimerekani nchini Iraq.

Waakilishi wa Baraza la kongress walipiga kura 221 wakiruhusu zitolewe pesa kiasi ya Dollar Billion 43 kati ya dollar billion 96 alizoomba Rais Bush kwa ajili ya Askari wa Mmerekani walioko nchini Iraq.

Spika wa chama cha Demokrat ambae pia ndie Spika wa bunge la kongress Bi Nancy Pelosi amesema enzi za Rais Bush kutaka cheki iliokua wazi kwa Askari wa Iraq sasa imekwisha.

Waakilishi 205 wametaka fedha hizo alizoomba Rais Bush zote zitolewe kwa pamoja.

Rais Bush akiwa katika shinikizo nyingi ametakiwa na Wabunge wa Demokrat kuyaondoa majeshi ya US nchini Iraq kwa muda wa miezi 6.

Lakini Rias Bush hilo halikumsumbua huku yeye akipanga Askari 30 elfu zaidi wa kimerekani wapelekwe nchini iraq.

Week iliopita Rais Bush kwa mara ya pili alipinga kwa kura yake ya veto, uamuzi wa Democrat kutaka Askari wa kimerekani laki moja na

arubaini na sita elfu (146,000) warejeshwe nyumbani ifikapo mwezi October .

Tayari Askari wa kimerekani 3379 wameshapoteza maisha yao nchini Iraq.

Mbunge wa chama cha Democrat senator Chuck

Schumer amesema , sasa Rais Bush anakabwa zaidi na vishindo kuliko Rais yoyote mwengine wa

Merekani tangu enzi za rais Richard Nixon.

Wakati huo huo Askari watatu zaidi wa kimerekani wameuawa nchini Iraq jana , na 9 kujeruhiwa vibaya, walipokua wakipiga doria katika eneo la

mkoa wa Diyala kaskazini mwa Iraq.

Hii imeifanya idadi ya Askari wa wakimerekani waliouawa nchini Iraq, kufikia watu 3385 tangu vita vya Iraq vilipoanza mwaka 2003.