1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush atembelea majeshi Kuwait

12 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Coal

KUWAIT.

Rais G.Bush wa Marekani leo anatarajiwa kuyatembelea majeshi ya nchi yake yaliyopo nchini Kuwait.Katika ziara hiyo rais Bush anaongozana na kamanda wa majeshi ya Marekani yaliyopo Irak jeneraali Petraeus.

Hapo awali rais Bush alifanya ziara nchini Israel na kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nane katika mashariki ya kati.

Juu ya mgogoro wa mashariki ya kati rais huyo ametabiri uwezekano wa kufikiwa suluhisho katika muda wa mwaka mmoja kabla ya kumaliza muhula wake wa urais , mwezi januari mwaka ujao.

Viongozi wa Israel na wa mamlaka ya Palestina wamesema utabiri wa rais Bush unatia moyo lakini gazeti la serikali la Syria Al-Thaura limesema maneno ya rais Bush hayana chochote.