1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush kuanza ziara yake ya Mashariki ya Kati wiki ijayo

6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ckvy

Rais George W Bush wa Marekani amesema ziara yake ya Mashariki ya Kati wiki ijayo inalenga kuziongezea nguvu juhudi za kuleta amani kati ya Israel na Wapalestina na kuvuruga malengo mabaya ya Iran.

Rais Bush ataondoka Marekani keshokutwa Jumanne kwenda Israel, kituo cha kwanza cha ziara yake. Kiongozi huyo atalitembelea eneo la Ukingo wa magharibi wa mto Jordan katika ziara yake ya kwanza katika eneo hilo.

Rais Bush amesema atamshinikiza waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas, waendeleze mazungumzo ya kutafuta amani yaliyoanzishwa tena kwenye mkutano uliofanyika mjini Annapolis katika jimbo la Maryland nchini Marekani.

Rais Bush atazuru pia Kuwait, Bahrain, jumuiya ya falme za kiarabu na Misri kabla kurejea mjini Washington mnamo tarehe 16 mwezi huu.