1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush kutoa maoni yake kuuokoa uchumi wa Marekani

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuGu

Rais George W Bush wa Marekani leo atatoa maoni yake kuhusu kuuimarisha uchumi wa nchi hiyo wakati bunge litakapojadili njia za kuzuia kuchuka kwa uchumi wa Marekani.

Makubaliano yamefikiwa kati ya chama cha Republican na chama cha Democratic, kuhusu haja ya kuwa na mpango wa kuuokoa uchumi ambao umeathirika kutokana na mikopo ya nyumba na kuongezeka kwa bei za mafuta.

Hata hivyo vipengele muhimu katika makubaliano hayo bado vinatayarishwa.