1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush ziarani Singapur

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCs9

Singapur

Rais George W Bush ameanza ziara ya wiki moja barani Asia hii leo akishadidia jukumu la kudumu la Marekani katika eneo hilo.Amesisitiza pia juu ya umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya ulinzi na biashara.Akizungumza mbele ya hadhara iliyokusanyika katika chuo kikuu cha Singapur hii leo rais George W. Bush amesema:

”Katika karne hii mpya,Marekani itaendelea kuwajibika barani Asia kwasababu masilahi yetu yanategemea kunawiri uhuru na fursa zilizoko katika eneo hili.Katika karne hii biashara yetu katika eneo la Pacific ni kubwa kuipita biashara tunayofanya katika eneo la Antlantic.”

Rais George W. Bush anatazamiwa pia kuhudhuria mkutano wa kilele wa jumuia ya ushirikiano wa kiuchumi ya nchi za Asia na pacific utakaoanza mwishoni mwa wiki hii mjini Hanoi nchini Vietnam.Mzozo wa kinuklea wa Korea ya kaskazini na juhudi za kupambana na ugaidi ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa.