1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Castro wa Cuba apata nafuu zaidi

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8U

HAVANA:

Rais Fidel Castro wa Cuba anaripotiwa kukutana na ujumbe kutoka China kwa muda wa saa nzima .Hii inaangaliwa kuwa ni ishara nyengine kwamba Kiongozi huyo anarejea katika afya njema.Rais Fidel Castro amekutana na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha kikoministi cha China, Wu Guanzheng.

China ni mshirika wapili mkuu wa biashara na Cuba baada ya Venzuela .Biashara ya pande hizo mbili ilifikia dala bilioni 2 mwaka jana.