1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Chavez atishia kuzuia kuiuzia mafuta Marekani

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVU4

Rais wa Venezuela,Hugo Chavez ametishia kuwa atasita kuizuia Marekani mafuta ikiwa Washington itajaribu kuchafua kura ya maoni juu ya mageuzi ya katiba.Ameituhumu Marekani kuwa inashirikiana na wapinzani wa sera zake za ndani.Chavez alitamka hayo alipohotubia mkutano wa hadhara katika mji mkuu Caracas.Vile vile aliwahimiza wananchi wenzake kuidhinisha mapendekezo ya mageuzi.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuondoa sheria inayomzuia rais kushika wadhifa huo kwa zaidi ya awamu mbili na pia kupunguza uhuru wa benki kuu ya Venezuela.Rais Chavez anasema,mageuzi hayo yatawapa wananchi mamlaka zaidi.Lakini wapinzani wake wanamtuhumu kuwa anajaribu kuimarisha mamlaka yake na kungángania madaraka.