1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Urusi zalaani mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya ulinzi ...

Mtullya, Abdu Said23 Mei 2008

Urusi na China zimelaani mpango wa Marekani wa kuweka mtandao wa ulinzi wa makombora barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/E53o
Rais Medvedev wa Urusi.Picha: AP

Rais Dmitry Medvedev wa Urusi na kiongozi wa China Hu Jintao  wamelaani mpango wa Marekani wa kuweka ulinzi wa makombora katika nchi  za Ulaya  ya mashariki.

Katika  tamko la  pamoja  mjini Beijing baada  ya rais Medvedev kuwasili China leo  viongozi  hao wamesema  mpango huo utarudisha nyuma juhudi za kupunga  silaha.

Katika tamko hilo China na Urusi zimesema mpango wa Marekani wa kuweka mtandao wa kimataifa wa ulinzi dhidi ya makombora hautasaidia kudumisha  urari  wa nguvu  za kijeshi na wala  hautasaidia kuimarisha  taratibu za kuzuia uenezaji  wa silaha za  nyuklia.

Rais Dmitry  Medvedev wa  Urusi amewasili  nchini  China kuanza ziara ya kwanza katika nchi  za  nje tokea aapishwe  kuwa  rais wa Urusi.

Ziara ya  siku mbili  ya  rais Medvedev nchini  China  ila lengo la kuimarisha ushirikiano katika  sekta  za kijeshi  na nishati. Na kwa ajili hiyo nchi hizo zimetiliana saini mapatano juu ujenzi wa kinu cha kuzalisha nishati ya nyuklia.

Mtambo huo utajengwa  kwa  thamani ya dola  za  kimarekani bilioni moja.