1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Erdogan kufanya ziara ya kwanza ya Misri leo

Sudi Mnette
14 Februari 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatazamiwa kuwasili mjini Cairo siku ya leo hii kukutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi.

https://p.dw.com/p/4cMlD
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan wa UturukiPicha: DHA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatazamiwa kuwasili mjini Cairo leo hii kukutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, na kuhitimisha juhudi za maelewano ya muda mrefu kati ya viongozi hao wawili. Awali Jumatatu ofisi ya Erdogan ilisema katika mkutano huo watazunguzia jitihada ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, wakati shirika la habari la Uturuki, Anadolu likisema mkutano huo pia utahusu masuala ya uchumi, biashara, utalii, nishati pamoja na  ulinzi. Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kwa rais wa Uturuki nchini Misri tangu mwaka 2012. Nchi hizo mbili zilivunja mahusiano mwaka 2013 baada ya Sisi, aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Misri, kumuondoa madarakani Hayati Mohamed Morsi, mshirika wa Uturuki na sehemu ya vuguvugu la Udugu wa Kiislamu.