1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Guinea Ikweta atoa msamaha kwa mwanaharakati

7 Juni 2012

Msamaha uliotolewa na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa guinea ya Ikweta kwa Dr Wenceslao Mansogo Alo mpinzani na mwanaharakati wa haki za binadamu umepongezwa na wanaharakati wa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/159uZ
Rais Guinea Ikweta
Rais wa Guinea IkwetaPicha: AP

Jambo la kuigwa huku wakiiomba serikali hiyo kumruhusu mganga huyo kuanza kutoa huduma ya tiba katika zahanati yake.

Taarifa ya kuachiwa kwa mpinzani huyo na mwanaharakati wa haki za binadamu ilitangazwa na Redio ya Serikali ya taifa la Guinea ya Ikweta jmapema juma hili ikisema kuwa Dr Mansogo na wafungwa wenzake kadhaa wamepata msamaha huo kutoka kwa Rais huyo aliyeko madarakani kwa muda mrefu.

Msamaha umetolewa wakati rais Mbasogo akisherehea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 70, Jumanne iliopita tarehe 5 Juni.

President Barack Obama stands during a family photo at the G20 Summit in Cannes, France, Thursday, Nov. 3, 2011. Bottom row, from left are: President Teodoro Obiang Nguema Mbasogo of Equatorial Guinea; Brazil President Dilma Rousseff; Russian President Dmitry Medvedev; Argentina President Cristina Fernandez; Chinese President Hu Jintao; French President Nicolas Sarkozy; President Barack Obama; Indonesian President Susilo Bambang Yudhoyono; Mexico President Felipe Calderon; South Korean President Lee Myung-bak; South Africa President Jacob Zuma. Middle row, from left are: European Commission President Jose Manuel Barroso; European Council President Herman Van Rompuy; Prime Minister Julia Gillard of Australia; Prime Minister Silvio Berlusconi of Italy; German Chancellor Angela Merkel; Prime Minister Recep Tayyip Erdogan of Turkey; Indian Prime Minister Manmohan Singh; Canada Prime Minister Stephen Harper; British Prime Minister David Cameron; Japanese Prime Minister Yoshihiko Noda. World Trade Organization Director General Pascal Lamy; World Bank Group President Robert Zoellick; President Khalifa bin Zayed Al Nahyan of the United Arab Emirates; Prime Minister Jose Luis Rodriguez Zapatero of Spain; Prime Minister Meles Zenawi of Ethiopia; Singaporean Prime Minister Lee Hsien Loong; United Nations Secretary General Ban Ki-moon; Internatinal Monetary Fund Managing Director Christine Lagarde; International Labor Organization Director-General Juan Somavia; OECD Secretary General Jose Angel Gurria. (AP Photo/Charles Dharapak)
Mojawapo ya mikPicha: dapd

Maamuzi haya yanakuja mwezi mmoja baada ya Dr Mansogo kufungwa huku wengine wakiwekwa ndani bila ya kupelekwa mahakamani. Akizungumzia hali hiyo mkurugenzi wa haki za binadamu kwa bara la Afrika Daniel Bekeke amesema kuwa tukio hili linaonyesha namna uhuru wa mahakama kutokuwepo.

Kukosekana kwa uhuru wa mahakama

Ameongeza kuwa Rais Obiang anasimamia serikali na mahakama na majaji wa taifa hilo kwenye kesi zinazogusa utawala na usalama wa taifa , wanaweka wazi kuwa kwanza huwa lazima wafanye mawasiliano na Ofisi ya Rais kabla ya kufikia maamuzi.

Japokuwa katiba ya Guinea ya Ikweta inaipa mahakama uhuru wake na kutoingiliwa lakini inaweka bayana kuwa rais ndiye Mkuu wa mahakama na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwateua majaji wanaotoa uamuzi wa kesi mahakakama kuu na uteuzi huo wa majaji hautahitaji kupitishwa na Bunge.

Mamlaka ya rais yanavuka mpaka hadi katika kamati maalumu ya majaji sita katika Baraza kuu la Majaji ambapo Rais ndiye mteuzi wa majaji wanaounda baraza hilo.

Dr Mansogo alikamatwa Februari 9 na Mei 7 akahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kile kilichoitwa uzembe. Lakini hukumu hiyo inatazamwa ilikuwa na ushawishi wa kisiasa ambapo Kiliniki yake ya tiba ilifungwa na akatakiwa kulipa Dola za kimarekani 10,000 kwa familia ya mgonjwa na kulipa faini ya dola 3000 kwa serikali. Kama hayo hayatoshi alifungiwa kujihusisha na matibabu kwa miaka 5.

Hali hii ni desturi kwa taifa hilo na mataifa mengi barani Afrika kwa kuwakandamiza wapinzani wale wanaonekana kuwa mwiba kwa serikali za nchi zao.

Msamaha huo kwa wafungwa umekuwa desturi kwa kiongozi huyo kwani Juni 2011 aliwaachia huru wafungwa 22 ambapo alikuwa anasherehekea sherehe yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 69.

Maoni ya Tutu Alicante

Akilitazama suala hilo kwa kina Tutu Alicante muanzilishi wa kituo cha haki za wale wanaoishi uhamishoni amesema taifa lao linatakiwa kuipa mahakama uhuru na na sio msamaha kutoka kwa rais.

Rais Obiang
Rais ObiangPicha: AP

Kwa pamoja Shirika hiolo la haki za binaadamu na shirika la haki za madaktari yameitaka serikali ya Guniea ya Ikweta kuruhusu kliniki ya Dr Mansogo kuanza kufanya kazi na kumruhusu kuanza kutoa tiba katika hospitali yake ambapo kibali chake cha kutibu kimezuiwa kwa miaka 5.

Wameongeza kuwa ni wajibu wa serikali hiyo kuheshimu taaluma ambazo zinatoa huduma kwa jamii.

Mwandishi:Adeladius Makwega/Htt://www.hrw.org/africa/equatorial-guinea.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman