1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Jammeh akabiliwa na upinzani mkali kwenye uchaguzi

Isaac Gamba
30 Novemba 2016

Uchaguzi wa urais nchini Gambia unafanyika Alhamis huku Rais Yahya Jammeh akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Adama Barrow kutoka chama cha United Democratic anayeungwa mkono na vyama vyengine.

https://p.dw.com/p/2TVcF
Yahya Jammeh
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Rais Jammeh anayelaumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika uongozi wake wa miaka 22, aligonga vichwa vya taarifa za vyombo vya habari duniani pale alipotangaza kuiondoa nchi yake kutoka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwezi Novemba.

Kiongozi huyo aliwahi pia kuitangaza kuwa nchi yake kuwa Jauhuri ya Kiisalamu na katika tukio jingine alisema ametengeneza dawa ya kutibu ugonjwa wa UKIMWI kwa kutumia kitabu kitakatifu cha Qur'an.  

Rais Yahya Jammeh alitwaa madaraka mwaka 1994 baada ya kumpindua Rais Dawda Jawara.