1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Köhler afanya ziara Afghanistan

21 Mei 2010

Rais wa Ujerumani Horst Köhler leo amefanya ziara ya ghafla isiyotarajiwa nchini Afghanistan, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Ujerumani kuizuru nchi hiyo katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.

https://p.dw.com/p/NU6Z
Rais wa Ujerumani Horst KöhlerPicha: picture-alliance/dpa

Mara ya mwisho kwa rais wa Ujerumani kuitembelea Afghanistan ilikuwa mwaka 1976 wakati huo rais akiwa Heinrich Lübke.

Rais Köhler akiongozana na mkewe Eva Luise aliwasili katika kambi ya wanajeshi wa Ujerumani kwenye mji wa Mazar-i-Sharif kaskazini mwa Afghanistan. Ziara ya Rais Köhler haikutangazwa kutokana na sababu za kiusalama.Aliwasili akitokea Shanghai China alikotembelea maonesho ya biashara duniani.

Dossier 1 Bundeswehr in Afghanistan
Majeshi ya Ujerumani katika mji wa Masar-i-Scharif kaskazini mwa AfghanistanPicha: AP

Katika ziara yake hiyo Kiongozi huyo wa taifa amewaambia wanajeshi wa Ujerumani kuwa, nchi yao inawaungaa mkono katika jukumu wanazofanya kuisaidia na kuijenga Afghanistan.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed