1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Karzai wa Afghanistan aongoza kwa kura zaidi ya asilimia 50

9 Septemba 2009

<p>Zoezi la kuhesabu kura nchini Afghanistan linaendelea kuleta hali ya kusisimua.

https://p.dw.com/p/JYgZ
Rais Hamid Karzai wa AfghanistanPicha: PA/dpa
Kwa  hivi  sasa  rais  wa  sasa Hamid  Karzai  rasmi  ametangazwa  kuwa  anaendelea kuongoza  mbele  ya mgombea  wa  karibu  yake  Abdullah Abdullah. Lakini  pamoja  na  hayo kuna  mapungufu mengi  yaliyojitokeza  katika  uchaguzi  huo. Taarifa  ya  Kai Küstner  inasomwa  studioni  na  Sekione  Kitojo.

Kwa  mara  ya  kwanza  katika  zoezi  hilo  la  kuhesabu kura  Hamid  Karzai  amefikia  hatua  ambayo  hakuna mgombea  mwingine  anayeweza  kuifikia  ya  zaidi  ya asilimia 50. Iwapo  hali  hiyo  itaendelea  ,  rais  huyo  wa sasa  tayari  atakuwa  amefanikiwa  katika  duru  ya kwanza  kupata  ushindi. Kama  tume   huru  ya  uchaguzi inavyoeleza, Karzai  hivi  sasa  ana  asilimia  54  ya  kura, na  mgombea  wa  karibu  Abdullah  Abdullah   anafuatia akiwa  na   zaidi  ya  asilimia  28. Wakati   kiasi  cha asilimia  90  ya  kura  zimekwisha  hesabiwa.

Je  hesabu  hii  ni  halali  kiasi  gani, kwa  kweli  hadi  sasa haifahamiki.  kwa  upande  mwingine  tume  ya  kusikiliza malalamiko, imeweka  kando  baadhi  ya  matokeo  hayo. Kama  anavyoelezea  muangalizi    wa  uchaguzi   huo ulioungwa  mkono   na   umoja  wa  mataifa , ameueleza uchaguzi  huo  kuwa  katika  uchunguzi  wao  imeonekana ushahidi  wa  kutosha  kuwa  kulikuwa  na  udanganyifu. Alim Seddiqi  msemaji  wa  umoja  wa  mataifa , amesema kuwa    matatizo  ya   kutokufuata  kanuni  yalikuwa makubwa.

Tunaitaka  tume  ya  uchaguzi  ya  Afghanistan  pamoja  na tume  ya  kusikiliza  malalamiko  kuongeza  juhudi  zao maradufu, ili  kuhakikisha  kuwa  kuna  juhudi  kubwa katika  kazi  zao  katika  kila  hatua. Hii  ni  pamoja  na kuondoa  kutoka  katika  matokeo  ya  mwisho  hesabu  ya masanduku  ambayo  yanadaiwa  kuwa  yalihusika  katika udanganyifu. Uhalali  wa  uchaguzi  huu  ni  muhimu  sana kwa  Afghanistan  na  washirika  wake  wa  kimataifa.

Shutuma  hizi  za  udanganyifu   zinaelekezwa   kwa upande  wa  Karzai. Taarifa  zinasema   kuwa  katika  jimbo moja   la  uchaguzi  rais  Karzai  amepata  asimilia  100  ya kura. Wagombea  wengine  wametoka  mikono  mitupu. Muda  mfupi  tu  baada  ya   uchaguzi  huo ,  taarifa zilieleza  kuwa  katika  kituo  kimoja  cha  uchaguzi masanduku  ya  kura  yamegunduliwa    yamejazwa    kura bandia. Gazeti  la  New York  Times  limeeleza  kuhusu mamia  ya  wapiga kura  hewa,  ambamo  wapiga  kura  laki moja  walijiandikisha  na  kumpigia     kura  Karzai, licha  ya kuwa hakuna  mtu  aliyepiga  kura  katika  eneo  hilo. Katika  jimbo  anakotoka  Karzai  la  Kandahar  kwa  mfano , matokeo  yanaonyesha  kuwa  kulikuwa  na  wapiga kura 350,000,  lakini  wachunguzi  wa  mataifa  ya  magharibi wameona  si  zaidi  ya  watu  25,000 , ambao  wamepiga kura  katika   jimbo  la  Kandahar.

Matokeo  halali  ya  mwisho  yatapatikana   iwapo  tuhuma hizo  za  udanganyifu  zitapatiwa  maelezo, na  wachunguzi wa  uchaguzi  huo  wanafikiria  kuwa  wiki  kadha  zitapita kabla  ya  kupata  jibu.

Pamoja  na  hayo  kuhusiana  na   jaribio  la   kupata maelezo  ni  pamoja   umoja  wa  mataifa, NATO   na serikali  ya  Afghanistan  kuhusiana  na  shambulio lililoamriwa  na  jeshi  la  Ujerumani   katika  jimbo  la Kunduz  Ijumaa  iliyopita. Katika  maelezo   yake  jeshi linaloimarisha  usalama  nchini  Afghanistan  limesema siku  ya  Jumanne, kuwa  matokeo  ya  uchunguzi  wake yanatarajiwa  baada  ya  wiki  kadha. Hii  ina  maana  pia kuwa  uchunguzi  unadhaniwa  kuwa  unaweza kuondolewa , kwasababu   katika  shambulio  hilo  pamoja na  wapiganaji  hata  raia  waliuwawa  na  wengine wamejeruhiwa.

Raia  pia  waliuwawa  katika  shambulio    la  hivi  karibuni kabisa  mjini  Kabul   jana  Jumanne.  Muuaji  aliwalenga wazi  wanajeshi  kutoka  nje, katika  lango  la  kambi  ya jeshi  iliyoko  katika  uwanja  wa   ndege   baada   ya kuilipua  gari  aliyokuwa  akiendesha. Taliban wanafahamika  kwa  mashambulio  haya. Mkuu  wa  kikosi cha  uhalifu  katika   jeshi  la  polisi  mjini  Kabul  amesema kuwa  watu  watatu  wameuwawa,  na  wengine  sita wamejeruhiwa.

Mwandishi  Kai Küstner / ZR / Kitojo, Sekione

Mhariri :Othman Miraji

: