1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kikwete akamilisha ziara yake nchini Burundi

22 Juni 2007

Rais Kikwete wa Tanzania amekamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Burundi.

https://p.dw.com/p/CHCN
Rais Kikwete amaliza ziara yake nchini Burundi
Rais Kikwete amaliza ziara yake nchini BurundiPicha: DW

Pamoja na kuwa na mazungumzo na serikali ya Burundi, Rais Kikwete amekutana pia na wafanyabiashara mashuhuri wa Burundi ambao amewaahidi kuwa nchi yake Tanzania itaazimia mikakati inayohitajika ili kuwarahisishia wafanyabiashara wa Burundi pindi bidhaa zao zinapopita kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Mengi zaidi anaripoti Amida Issa kutoka Bujumbura.