1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kikwete kuapishwa leo

Kabogo Grace Patricia6 Novemba 2010

Rais Kikwete anaapishwa kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya kushinda katika uchaguzi wa Jumapili iliyopita.

https://p.dw.com/p/Q0IG
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.Picha: DW

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete anaapishwa hii leo kuiongoza nchi hiyo katika kipindi cha pili cha miaka mitano, baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa-NEC ilitangaza matokeo hayo hapo jana ambapo ilisema Rais Kikwete ameshinda kwa kupata asilimia 61 ya kura, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Hata hivyo, kiongozi wa upinzani kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Dr. Wilbrod Slaa anataka kura zihesabiwa tena kwa madai kuwa kulifanyika udanganyifu.

Chama tawala cha Rais Kikwete cha CCM, kimekuwa madarakani tangu Tanzania ilipopata uhuru wake mwaka 1961.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (DPAE,RTRE)

Mhariri: Sekione Kitojo