1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Lahoud aondoka Ikulu.

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSc0

Beirut. Rais Emile Lahoud wa Lebanon ameondoka kutoka katika jumba la rais mjini Beirut kwa mara ya mwisho kama mkuu wa nchi. Rais huyo anayeiunga mkono Syria aliondoka madarakani bila ya kupatikana kiongozi wa kuchukua nafasi yake. Juhudi za hivi karibuni za bunge la nchi hiyo kumchagua rais mwingine zilishindwa saa chache hapo kabla , baada ya kikao cha uchaguzi kususiwa na kambi ya upinzani inayounga mkono Syria kwa kulinyima bunge idadi ya wabunge wanaotakiwa kupiga kura. Saa chache kabla ya kuondoka madarakani , rais Lahoud alikabidhi madaraka kwa jeshi la usalama la nchi hiyo. Waziri mkuu Fouad Siniora , ambaye serikali yake haikuwahi kutambuliwa na rais huyo wa zamani , amesema kuwa uamuzi huo haukuwa katika misingi ya katiba. Waziri mkuu anayeipinga Syria pia amesema kuwa chini ya katiba ya nchi hiyo , baraza lake la mawaziri litakuwa kwa muda madarakani.