1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais mpya kupatikana Ijumaa.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW3U

Beirut.Nchini Lebanon juhudi za kumpata rais mpya zinaonekana kumalizika , baada ya wabunge wanaounga mkono mataifa ya magharibi wenye wingi mkubwa kumteua rasmi kamanda wa jeshi la nchi hiyo jenerali Michel Suleiman kuwa mgombea wa kiti hicho.

Hali ya kutokuwa na uongozi wa juu ilijitokeza baada ya muda wa utawala wa rais Emile Lahaoud ulipomalizika hapo Novemba 24 bila kupatikana rais mpya.

Wabunge wanatarajiwa kumchagua Suleiman kuwa rais siku ya Ijumaa.