1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mubarak yuko tayari kwa mazungumzo

4 Februari 2011

Makamu mpya wa Rais nchini Misri Omar Suleiman, ametangaza kuwa Rais Hosni Mubarak anayepingwa amesema yuko tayari kwa mazungumzo na makundi ya wapinzani.

https://p.dw.com/p/10ATV
Rais Hosni Mubarak wa MisriPicha: picture-alliance/dpa

Matamshi hayo ameyatoa wakati ambapo mapigano kati ya waandamanaji wanaoiunga mkono serikali ya Misri na wale wanaoipinga yakiendelea kwa siku ya kumi kwenye mji mkuu wa Cairo.

Hata hivyo, ahadi hiyo ya Rais Mubarak imekataliwa na chama cha upinzani kilichopigwa marufuku nchini Misri cha Muslim Brotherhood.

Muslimbruderschaft Ägypten Pressekonferenz
Viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood nchini MisriPicha: picture-alliance /dpa

Wakati huo huo, gazeti la New York Times linaripoti kuwa serikali ya Rais Barack Obama wa Marekani inajadiliana na maafisa wa Misri kuhusu pendekezo la Rais Mubarak la kujiuzulu haraka na kuibadilisha serikali kuwa ya mpito ikiongozwa na Makamu wa Rais, Omar Suleiman.

Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 300 wameuawa nchini Misri tangu machafuko ya wenyewe kwa wenyewe yalipoanza.

Mwandishi:Grace Patricia Kabogo

Mpitiaji:Hamidou Oummilkheir