1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Muisharraf aapishwa kua rais wa kiraia wa Pakistan

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUdL

Islamabad:

Pervez Musharaf ameapishwa rasmi hii leo kushika hatamu za uongozi wa Pakistan kwa kipindi chengine cha miaka mitano,kama rais wa kiraia.Hafla hiyo imefanyika siku moja tuu baada ya rais Musharaf kuyapa kisogo madaraka yake kama kiongozi wa vikosi vya wanajeshi..Rais Musharaf anasema:

“Hii ni siku ya kihistoria kwangu ni siku ya hisia kubwa kwangu na mni siku inayofungua ujia ya kuingia katika demokrasia kamili.”

Marekani na upande wa upinzani nchini Pakistan wanamshinikiza Pervez Musharaf abatilishe pia sheria ya hali ya hatari kabla ya uchaguzi wa bunge kuitishwa january nane mwakani .

Wakati huo huo bomu lililotegwa barabarani katika mji wa karibu na Miran Shah limegharimu maisha ya wanajeshi watano na wengine kadhaa kujeruhiwa.Mji huo unakutikana katika jimbo la machafuko la kaskazini la Waziristan linalopakana na Afghanistan.