1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Musharraf asema huenda Benazir Bhutto alipigwa risasi

6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ckvz

Rais wa Pakistan Pervez Musharraf amesema kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto, aliyeuwawa kwenye mkutano wa kampeni mnamo tarehe 27 mwezi uliopita, huenda alipigwa risasi.

Akizungumza kwenye mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la kimarekani, CBS, yatakayotangazwa hii leo, rais Musharraf amesema marehemu Bhutto alikuwa na usalama wa ziada na hakutakiwa kusimama nje ya gari lake.

Aidha kiongozi huyo amekiri wachunguzi wa kifo cha Benaziri Bhuto huenda walipitisha uamuzi kwa haraka na kuharibu ushahidi.

Hata hivyo amesisitiza serikali yake ina uwezo wa kuendesha uchaugzi huo ikisaidiwa na polisi wa kupambana na ugaidi kutoka Uingereza ambao wamo nchini Pakistan.