1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Musharraff kuhutubia Taifa

2 Januari 2008

Chama cha Pakistan Peoples' Party chapinga kuahirishwa uchaguzi wa januari 8.

https://p.dw.com/p/Cj7F

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan analihutubia Taifa hii leo.Katika hotuba yake hiyo ambamo anatazamiwa kuahirisha uchaguzi uliopangwa Januari 8, anatarajiwa pia kuwataka wapakistan kuonesha umoja na utulivu kufuatia kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto.

Chama cha marehemu :Pakistan Peoples’ Party kinapinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo na kinadai ufanywe kama ilivyopangwa.

Ikiwa afisi kadhaa za uchaguzi zimeteketezwa katika machafuko yaliofuatia kuuwawa kwa Bibi Benazir Buhtto,maafisa wa Tume ya Uchaguzi wanadai uchaguzi wa Januari 8 uahirishwe hadi mwezi ujao wa Februari.

Mjumbe wa chama cha upinzani cha Pakistan Peoples’ party akipinga shauri hilo alisema:

„Ningependa kuwakumbusha kuwa orodha za majina ya wapigakura zimeorodheshwa katika komputa na ni suala la dakika 25 tu kuzichapisha na pia ni swali la nusu siku tu kuzieneza katika afisi chache ambako kuna hisia za shaka-shaka.“

Mjumbe huyo wa Pakistan Peoples’ party akaongeza kusema:

„Kwahivyo, chama cha Pakistan Peoples’ party kina hamu kuona uchaguzi unafanyika kwa wakati uliopangiwa-yaani januari 8.“

Kila uchaguzi uliofanyika karibuni nchini Pakistan-dola pekee la silaha za kinuklia la kiislamu ,ukigubikwa na tuhuma za kupitishwa mizengwe na udanganyifu na chama cha Bhutto kimetuhumu hapo jana kwamba kucheleweshwa kokote kufanyika uchaguzi uliopangwa ni ujanja wa kuwapa washirika war ais Musharraf muda wa kufanya njama za kwiba kura.

Tume ya Uchaguzi nchini Pakistan imedai maandalio ya uchaguzi yamekwamishwa na machafuko yaliozuka kufuatia kuuwawa kw Benazir Bhutto.

Vyama vya Upinzani vinatuhumu kwa upande wao kwamba Tume ya uchaguzi imejazwea wafuasi war ais Musharraf na kuwa serikali ya mpito ilioteuliwa kuiongoza Pakistan wakati huu kuelekea uchaguzi pia inampendelea rais Musharraf.

Marekani inayoiangalia Pakistan kama mshirika wake wa chanda na Ptee katika vita dhidi ya ugaidi,imesema kuichelewesha uchaguzi kutakubalika tu iwapo vyama vikuu vya kisiasa nchini Pakistan vitahusishwa katika kupitisha uamuzi huo.

Chini ya hali hii, rais Pervez Musharraf anatazamiwa kulihutubia taifa hii leo akitazamiwa kutoa mwito wa kuwapo utulivu na umoja nchini Pakistan.Atajaribu kuzima jaziba katika wiki iliojionea kuuwawa hadi wa tu 60 kutokana na jazba ya kifo cha Benazir Bhutto.

Serikali ya Musharraf inawalaumu magaidi wa Al Qaeda kuandfaa njama ile ya kumua Benazir Bhutto wakati wa kampeni ya uchaguzi.

Video zilizoonesha shambulio la kuuwawa kwa Benazir Bhutto zimezusha shaka shaka juu ya tafsiri iliotolewa na serikali .Al Qaeda nayo imekanusha kuhusika na kifo hicho.

Rais Musharraf amekabiliwa na vilio kutoka chama cha Bibi Benazir Bhutto na wanasiasa fulani nchini Marekani kuruhusu

uchnguzi wa kimataifa .Haijulikani iwapo,rais Musharraf katika hotuba yake ya leo kwa taifa atajibu juu ya dai hilo.