1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Nkurunziza atakiwa kuahirisha uchaguzi

Admin.WagnerD7 Julai 2015

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamemtaka rais Nkurunziza kuahirisha uchaguzi wa kwa muda wa wiki mbili, kufuatia maandamano yanayoendelea ya kupinga hatua ya Nkurunziza kuwania mhula wa tatu madarakani.

https://p.dw.com/p/1FttL
Pierre Nkurunziza
Rais Pierre NkurunzizaPicha: I.Sanogo/AFP/GettyImages

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu umependekezwa ufanyike tarehe 30 mwezi huu wa Julai. Mkutano wa kilele ulioitishwa nchini Tanzania ambapo marais wa Kenya, Rwanda na Burundi walituma tu wawakilishi umemteua rais Yoweri Museveni wa Uganda kuwa mpatanishi kati ya serikali ya Burundi na Upinzani. Amina Abubakar amezungumza na Felix Nzoru-bo- nanya, kutoka Shirika la Haki za Binaadamu nchini Burundi na kwanza alimuuuliza juu ya nafasi ya Rais Museveni kufanikiwa katika juhudi hizo za upatanishi?

Mwandishi :Amina Abubakar

Mhariri :Mohammed Abdul-Rahman